33.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI, CHADEMA WATOFAUTIANA MGOMBEA KUSHAMBULIWA ARUSHA

|Mwandishi Wetu, Arusha



Uchaguzi mdogo wa Kata ya Kaloleni Jimbo la Arusha umeingia dosari baada ya kuibuka vuruga na baadhi ya watu akiwamo mgombea wa kata hiyo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kudaiwa kuchomwa kisu na kujeruhiwa shingoni na kwenye taya na watu wanaosadikiwa kuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mbali ya vurugu hizo gari la mgombea wa Kata ya Daraja Mbili Masoud Sungwa lilidaiwa kutobolewa tairi la nyuma kulia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhan Ng’anzi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema hakuna mgombea aliyechomwa kisu katika Kata ya Kaloleni.

“Kilichotokea ni kwamba mgombea wa kata hiyo ameshambuliwa na watu wasiojulikana na sasa hivi tumefungua kesi ili kuanza uchunguzi.

“Aliyechomwa kisu ni mwanachama wa CCM, ambaye alichomwa kisu eneo la Mianzini baada ya kukutana na kundi jingine ukatokea mzozo baina ya makundi hayo mawili ambapo mmoja kati ya makundi hayo akachomoa kisu akamchoma na aliyefanya hivyo tunamshiklilia hapa kituoni kwa mahojiano zaidi, lakini kwa ujumla uchaguzi katika mkoa wetu unaendelea vizuri, usalama po wa kutosha.

Wakati huo huo, Chadema kimetangaza kujitoa katika uchaguzi wa Kata ya Songoro, kutokana na mgombea wake na mawakala wake kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles