Rais Joseph Kabila wa Congo hatogombea tena urais na kwamba chama chake kimemchagua Emmanuel Ramazani Shadari kuwa mrithi wake na mgombea wa uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali, Lambert Mende, Shadari amekwisha wasilisha stakhabadhi zake za kuwania urais kwa Tume ya Uchaguzi mchana wa leo.
Shadari mwenye umri wa miaka 57 alikuwa Katibu wa kudumu wa Chama Tawala cha PPRD, mtu wa karibu na wa muhimu wa kampeni za Rais Joseph Kabila.
Kutangazwa kwa mgombea urais mpya ni tukio ambalo limeondoa shaka ambayo wengi walikuwa nayo kuwa huenda Rais Kabila akakataa kuwepo kwa ukomo wa urais.
“Jahmuri ya Kidemorisia ya Congo ni nchi inayoongozwa na katiba hatujakiuka katiba na tutaendelea kuiheshimu. Kwa mda huu kilicho muhimu ni kuangalia maisha ya wakongo,” alisema Kabila.