24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

SHIBUDA AMTAKA BASHIRU ALLY KUWADHIBITI WANAOTAFUTA ‘KIKI’

|Bethsheba Wambura, Dar es SalaamMwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini,  John Shibuda, amemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally kuwadhibiti watumishi wa Serikali wanaoibua mambo na kuyatenda kwa kutafuta ‘kick’ za kisiasa kinyume na amri ya Rais John Magufuli.

Amesema tabia za namna hiyo zikiachwa zikazoeleka katika jamii na watu wakatambua kuwa yeye (Rais) ndiyo anatoa amri hizo kumbe siyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatano Agosti 8, katika mkutano wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini, Shibuda amesema baadhi ya maagizo mengi yanayotolewa na viongozi si amri za Rais Magufuli.

“Namuomba Dk. Bashiru awadhibiti watumishi wa serikali wanaotafuta kiki za kisiasa kwa wanaoibua mambo ambayo hayana amri za Rais Magufuli na kujijengea umimi na usisi, mkiondoa hilo mtakuwa mnajenga taswira njema.

“Na msiache tabia zenye kujenga kasoro na kuibua hitilafu dhidi ya rais zikazoeleka ndani ya jamii na watu wakatambua kuwa yeye ndiyo anatoa amri hizo ila kwa ufahamu wangu naamini kuwa baadhi ya mambo yanayosemwa hayatoki kwake,” amesema Shibuda.

Amewataka watumishi hao kuacha kumbebesha mambo ambayo si ya kwake wakidhani kufanya hivo wataifurahisha jamii na kumfurahisha Rais Magufuli mwenyewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles