25.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

MASHINE FEKI 45 ZA MICHEZO YA KUBAHATISHA ZATEKETEZEZWA

Janeth Mushi, Arusha

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini (GBT) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, limekamata na kuteketeza mashine feki 45 zenye thamani ya Sh milioni 90, za michezo hiyo zilizoingizwa nchini kinyemela.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Julai 26, Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi amesema mashine hizo zilikutwa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha katika operesheni iliyofanyika kwa kipindi cha wiki moja.

Amesema katika operesheni hiyo waliwakamata watuhumiwa wawili akiwamo raia mmoja wa China na Mtanzania mmoja ambapo upelelezi wa watuhumiwa wengine unaendelea.

“Tumebaini kuwa mashine hizo hazikufuata utaratibu ikiwamo kutosajiliwa kutumika hapa nchini na kutolipiwa kodi huku zikitumika katika maeneo ambayo hayajaidhinishwa na bodi hiyo,” amesema.

Kwa upande wake, Meneja wa Ukaguzi na udhibiti wa bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Sadick Elimsi, amesema awali bodi hiyo ilipata taarifa za kuingizwa kinyemela kwa mashine hizo bila kufuata utaratibu wa usajili huku baadhi yake zikiwa ni feki.

“Mashine hizi zinapoingia nchini huwa tunaziweka alama maalumu za utambuzi ambazo zinaonyesha zinastahili kutumika nchini na zimesajiliwa na bodi hiyo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles