30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

JPM AFICHUA MAKAMPUNI YANAVYOKWEPA KODI

CHETI: Rais Dk. John Magufuli, akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali George Waitara, kutambua mchango wa shirika hilo baada ya kuvuka lengo la gawio lao kwa serikali, Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo, Dk. Allan Kijazi. Picha na Loveness Bernald


ANDREW MSECHU Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM |


RAIS Dk. John Magufuli, ametaja njia kuu tatu zinazotumika na makampuni ya nje kukwepa kodi na kutoa gawio kwa Serikali, huku akiiagiza Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kudhibiti mianya hiyo.

Rais Magufuli alisema hayo Dar es Salaam jana wakati wa kupokea gawio la Sh bilioni 736.36 kutoka kwa wakala, taasisi, kampuni na mashirika ya umma 43, ambapo alisema baadhi ya kampuni zina kampuni zake tanzu au kampuni mama, ambazo hutumika kukwepa kodi, tozo, malipo ya mrabaha na gawio.

Alisema hana tatizo na suala la kampuni kuwa na kampuni tanzu au kampuni mama nje, lakini tatizo lake ni pale kampuni hizo zinavyotumika kufanya udanganyifu.

Alisema njia ya kwanza inayotumika ni kuongeza gharama za uendeshaji kwa lengo la kupunguza kiwango cha faida ili kampuni za hapa nchini zionekane zinafanya vibaya au kupata hasara.

“Hii kitaalamu inaitwa transfer pricing. Ujanja huu hutumika katika kuagiza vifaa na vipuri ambapo kampuni zilizopo nchini huagiza vifaa kwa kutumia kampuni tanzu ambazo huuza vifaa hivyo kwa kampuni za hapa nchini kwa bei ya juu hata mara mia moja zaidi ya bei halisi.

“Kwa kuwa sheria zetu za kodi na uwekezaji hutoa misamaha ya kodi gharama hizo huendelea kukatwa kwa mapato ya kampuni hizo miaka yote hivyo kuzifanya zisilipe kodi wala gawio.

“Kampuni zilizopo nchini huchukua mikopo kwa riba kubwa kutoka kampuni tanzu nje ya nchi na kuongeza gharama za uendeshaji na kuzifanya kampuni hizo zionekane zinapata hasara hivyo kuzifanya zisilipe kodi, lakini licha ya kupata hasara kampuni hizo zinaendelea kuwepo,” alisema.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles