21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

KANGI LUGOLA AMSWEKA ASKARI MAHABUSU ARUSHA

                                                                  |Eliya Mbonea, Arusha


Askari Polisi mmoja wa Kituo cha Utalii na Diplomasia Mjini Arusha, leo amejikuta akizindua mahabusu ya kituo hicho kwa kuwekwa mahabusu kwa agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola.

Kituo hicho kilizinduliwa na Rais John Magufuli mapema mwaka huu ambapo tangu wakati huo hakijawahi kupokea mahabusu yeyote.

Waziri Lugola, ametoa agizo hilo leo Jumatatu, Julai 23 alipotembelea kituo hicho cha kisasa, ambapo akiwa hapo alimuhoji baadhi ya mambo kadhaa ambayo askari huyo alishindwa kuyajibu kwa ufasaha.

“Nimeingia kwenye chumba cha mashtaka, nikamkuta askari nikamuuliza vitabu muhimu kwenye chumba hicho akabaki ameduwaa, nikamuagiza RPC (Kamanda wa Polisi) amuweke ndani. Lakini baadaye nikaamuru atolewe kwani yawezekana askari huyo hana elimu ya masuala ya utalii,” amesema.

Amesema kama kituo hicho hakijawahi kuweka mahabusu mtu, basi askari huyo amekuwa wa kwanza kukifungua kwa kukaa mahabusu,” amesema Waziri Lugola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles