Na MOHAMED HAMAD-MANYARA
IDARA ya Uhamiaji wilayani Kiteto, imeanza uhakiki wa uraia kwa watu zaidi ya 1200 wanaoshi katika Kata ya Sunya.
Kazi hiyo ni mwendelezo wa hatua ya awali ya kuhakiki walowezi walioingia nchini kabla ya Uhuru mwaka 1961 hadi mwaka 1972, wao na vizazi vyao.
Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu, Mkuu wa Uhamiaji Wilaya ya Kiteto, Ikomba Mathew, alisema kazi hiyo inafanyika ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Uhamiaji sura 54 rejeo la mwaka 2016 na kanuni zake, pamoja na maelekezo ya Rais Dk. John Magufuli.
“Sheria ya Uhamiaji inatambua uwepo wa wahamiaji walowezi na vizazi vyao na kuwataka waishi nchini kwa mujibu wa sheria,” alisema Ikomba.