Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Siku chache baada ya kutoa utafiti wake, Taasisi isiyo ya Serikali ya Twaweza imeandikiwa barua na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) ikitakiwa kujieleza ndani ya siku saba ni kwa nini isichukuliwe hatua za kisheria kwa kufanya na kutoa matokeo ya utafiti kuhusu maoni ya wananchi bila kibali.
Kwa mujibu wa barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na Mkurugenzi wa Costech, Amos Nungu imesema Twaweza waliwasilisha maombi ya vibali vya kufanya utafiti wa awali nchini lakini utafiti huo wa Sauti ya Wananchi haukuwasilishwa katika maombi yao.
Soma zaidi… http://mtanzania.co.tz/wameporomoka/
“Matokeo ya utafiti huo yanakiuka kifungu cha 11 cha Mwongozo wa Kusajiliwa na Kuidhinishwa kwa Usajili wa Kitaifa kwa kutoandikisha mradi huu wa utafiti kwa Costech,” imesema sehemu ya barua hiyo.
Katika utafiti huo wa Twaweza, matokeo yalionyesha kuporomoka kwa umaarufu wa rais, vyama vya siasa, wabunge na madiwani.