29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Julius Mtatiro rasmi Segerea

mtatiroNa Elizabeth Hombo, Dar es Salaam

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimemteua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro kuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam.

Hatua ya kuteuliwa kwa Mtatiro kuwania ubunge katika jimbo hilo imefuta ndoto za baadhi ya makada wa Chadema ambao walikuwa wakitajwa kutaka kuwania jimbo hilo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana alisema ameteuliwa kuwa mgombea na amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi wa Manispaa ya Ilala.

“Ndugu zangu, leo chama changu kimenipa ridhaa na barua rasmi ili nigombee ubunge kwa tiketi ya UKAWA, nimetoka kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Segerea.

“Natumaini kuwa tutaanza kwa nguvu na kumaliza kwa ushindi. Nawaahidi kuwa nitaunganisha vyama vya CUF, CHADEMA, NCCR na NLD kushirikiana na wananchi wa Segerea kupata madiwani wa kata zote 13. Historia yangu imekuwa ya mapambano ya kudai haki za wanyonge, nitaendelea hivyo hadi mwisho wa pumzi za uhai wangu,” alisema Mtatiro.

Alisema ameishi Segerea kwa miaka 12, ana uzoefu wa kutosha na changamoto za wananchi wa Segerea na ameziishi na sasa anahitaji kuungwa mkono ili ashirikiane na wanachi kuzitatua na kuwapigania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles