24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi wawakamata walinzi wa Chadema

msangiNA PENDO FUNDISHA, MBEYA

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa vijana wa kikosi cha ulinzi   cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), red brigade.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema mjini hapa jana kwamba vijana hao ni kati ya waliokuwa wamevaa nguo nyeusi, kofia na viatu vyeusi wakati wa mapokezi ya mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowassa  mjini Mbeya wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Kamanda Msangi, vijana hao walikuwa na mwonekano kama askari na shughuli walizokuwa wakifanya wakati wakiwaongoza wananchi kumpokea Lowassa walionekana kama askari wenye mafunzo.

“Hawa vijana siku hiyo walikuwa wakiongoza msafara, walikuwa wakifanya ulinzi na kazi nyingine za Jeshi la Polisi.

“Kutokana na mwonekano wao na shughuli walizokuwa wakizifanya, ilitafsiriwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi waliokuwa wakifanya kazi katika mapokezi hayo.

“Kwa hiyo kutokana na sintofahamu hiyo, wananchi wengi walikuwa wakihoji hilo ni jeshi gani na wengine walikuwa wakituma picha za vijana hao kwenye mitandao ya jamii wakionyesha wasiwasi wao kuhusu kikundi hicho,”alisema Msangi.

Msangi alisema ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai  Mkoa wa Mbeya, ilifungua jalada la uchunguzi   kuwapata vijana hao kuwahoji na kukamilisha upelelezi  jalada lipelekwe kwa mwanasheria wa serikali kwa ufafanuzi wa sheria.

“Hatua hii imechukuliwa kutokana na kuibuka   makundi ya aina hii hasa kwa vyama vikubwa vya siasa   nchini. Katika kufanya ufuatiliaji wetu  vijana wawili walikamatwa alfajiri ya leo (jana) kwa mahojiano na baada ya maelezo yao kuchukuliwa walidhaminiwa,” alisema Kamanda Msangi.

Hata hivyo, hakutaja majina ya watuhumiwa hao kwa kile alichosema upelelezi bado unaendelea.

Kamanda Msangi alivitaka vyama vya siasa kufuata taratibu za vyama vyao zitakazokuwa haziingiliani na taratibu za Jeshi la Polisi wala jeshi lolote nchini.

Wakati Lowassa anawasili mjini Mbeya wiki iliyopita akiwa ameongozana na viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vijana hao walikuwa wakiongoza msafara wa mgombea urais huyo.

Kutokana na ulinzi uliokuwa ukiimarishwa na vijana hao, baadhi ya wananchi walishindwa kuwaelewa kwa kuwa walikuwa wakifanya ulinzi kwa weledi wa hali ya juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles