27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

NSSF WATAKIWA KUTENGA DIRISHA LA UKIMWI

CHRISTINA GAULUHANGA NA TUNU NASSOR


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Sera, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenister Mhagama, ameliagiza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuhakikisha linatenga dirisha maalumu la kupima virusi vya Ukimwi ili kuunga mkono jitihada za Serikali za kutokomeza ugonjwa huo.

Akizungumza katika maonyesho ya 42 ya Sabasaba, Jenista alisema  kufunguliwa kwa dirisha hilo kutasaidia wananchi wengi kujitokeza kupima afya zao.

Alisema ni vyema uongozi wa NSSF ukafanya jitihada za kuwashirikisha wataalamu wa afya ili kufungua dirisha hilo litakalosaidia wananchi wengi kufahamu afya zao.

“Naomba ndugu zangu wa NSSF kuhakikisha mnafungua dirisha la kupima afya katika maonyesho haya ya Sabasaba, tena viongozi wa NSSF muwe wa kwanza,” alisema Jenista.

Alisema kuna utamaduni umejengeka kwa wanaume wengi kukataa kupima afya zao, jambo ambalo limekuwa likichangia kukosekana kwa takwimu za walioathirika na ugonjwa huo.

Alisema kupima afya hasa virusi vya Ukimwi ni uhodari na mwanamume yeyote anayepima kwa hiari anaonyesha umakini wake.

Jenista aliipongeza NSSF kwa kutoa mafao ambayo yamesaidia kuchagiza sekta mbalimbali kujiimarisha.

Pamoja na hali hiyo, aliitaka NSSF kujenga utamaduni wa kulipa mafao kwa wakati ili wananchi wanufaike na mfuko huo.

Alisema utafiti uliofanywa unaonyesha NSSF ina uwezo wa kujiendesha kwa miaka 70, hivyo ni imani ya Serikali kuwa itaweza kufikisha huduma za jamii moja kwa moja.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara,  alisema atafungua dirisha la kupima afya na atakuwa wa kwanza kupima.

Alisema NSSF imejipanga kuhakikisha jamii inafikiwa kirahisi na ndio sababu ya kupewa ushindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles