25.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

MA-DC, WAKURUGENZI WATAKIWA KUTOA ELIMU TOZO BIDHAA ZA NJE

Hadija Omary, Lindi

Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wenyeviti wa Halmashauri Mkoani Lindi wametakiwa kuwaelimisha wananchi wa maeneo yao juu ya  tozo ya bidhaa zinazosafirishwa nje ya nchi (export levy) katika zao la korosho.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alipokuwa anazungumza na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Manispaa hiyo leo.

Zambi amesema wananchi wanapaswa kufahamu kuwa tozo ya  bidhaa zinazosafirishwa nje ya nchi katika zao la korosho ni ushuru anaotozwa mnunuzi wakati wa kusafirisha zao hilo na si miongoni mwa tozo anazotozwa mkulima wakati anauza korosho zake.

“Suala hili inaonyesha kama vile serikali inawaibia ama kuwanyang’anya wakulima fedha zao, jambo hili ukiliangalia kwa mapana ni kama vile linawagombanisha wakulima na serikali yao.

“Ili kusawazisha jambo hili ni vyema tukashirikiana kwa pamoja kupitia vikao na mikutano na wananchi na wakulima  wetu tukaweka ajenda ya jambo hili katika mazungumzo na watu wetu ili waweze kufahamu,” aliongeza Zambi.

Amesema Wakulima wanapaswa kufahamu kuwa tozo hiyo anakatwa mnunuzi ambapo mkusanyaji wa tozo hiyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na inakwenda katika mfuko mkuu wa serikali ambapo asilimia 65 ya fedha hiyo huenda kwenye  mfuko wa kuendeleza zao la korosho (mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao la korosho) na asilimia 35 zinabaki mfuko mkuu wa serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles