21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

UNDP YAIPIGA JEKI YA UMEME WA JUA ZAHANATI LINDI

Hadija Omary, Lindi

Wajawazito na wagonjwa mbalimbali katika Zahanati ya Rondo Junior Seminary, iliyopo Kitongoji cha Ngara, kijiji na Tarafa ya Mnara, mkoani hapa wameondokana na adha ya kutumia vibatari wanapolazwa au kupatiwa matibabu usiku katika hospitali hiyo baada ya kuwekewa umeme wa  nishati ya jua (Solar) kwa ufadhi wa Shirika la Maendeleo la Umoja   wa Mataifa (UNDP).

Hayo yameelezwa na muuguzi wa zahanati hiyo, Judith Mbaya alipokuwa akitoa maelezo ya zahanati hiyo mbele ya ujumbe kutoka UNDP, ulipotembelea chuoni hapo, kuona misaada waliyoifadhili namna inavyofanya kazi.

Judith amesema tangu kupatikana kwa nishati hiyo kumerahisisha upatikanaji wa huduma ndani ya seminari hiyo na kwa wakazi wa jirani na hasa kwa akina mama wajawazito wanaokwenda kupata huduma.

“kabla ya kupata nishati hii tulikuwa tunalazimika kutumia vibatari au tochi wakati wa kumsaidia mama mjamzito wakati wa kujifungua jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa mtoto na mama mwenyewe,” amesema Judith.

Aidha, amesema licha ya zahanati hiyo  zahanati kuhudumia wafanyakazi wanaoishi katika seminari hiyo pia hutoa huduma kwa wakazi wengine zaidi ya 700 wanaoishi katika vijiji jirani.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, amepongeza namna ya fedha waliyoitoa kwa ajili ya kuteleleza miradi katika zahanati hiyo inavyotumika ipasavyo ambapo pia amewaasa wahudumu wa zahanati hiyo kutunza miundombinu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles