25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Simba ‘yamvua nguo’ Ivo

Kipa wa Simba, Ivo Mapunda
IVO MAPUNDA

NA MWANDISHI WETU

ALIYEKUWA kipa wa timu ya Simba, Ivo Mapunda, amegeuziwa kibao na uongozi wa timu hiyo baada ya kuambiwa arudishe sehemu ya kitita cha fedha alichopewa kwa ajili ya kusaini mkataba mpya.

Ijumaa iliyopita gazeti hili liliripoti kuwa uongozi wa timu hiyo umesitisha mpango wa kumwongezea mkataba kipa

huyo kwa mizengwe, ikidaiwa hawana imani naye tena, licha ya awali kufanya naye mazungumzo na ikadaiwa alitanguliziwa kitita cha Sh milioni 10 kama kishika uchumba.

Hata hivyo, tangu hapo hakuwahi kupewa karatasi za mkataba ili amalizie taratibu za kusaini, lakini uongozi wa Simba umekuwa ukidai kuwa mkongwe huyo amekuwa akiwakimbia jambo ambalo lilipingwa na kipa huyo akisema hakuwahi kupewa mkataba na mabosi wake.

Ivo aliliambia MTANZANIA jana kuwa atarudisha fedha hizo kama alivyotakiwa baada ya zoezi la kuongezewa mkataba kusitishwa.

“Sitaweza kuweka wazi nitazirudisha lini, ni kweli walinipa fedha baada ya makubaliano ya awali na mimi nikazipeleka kufanyia biashara, hivyo nitazirudisha tu mambo yakikaa vizuri,” alisema.
Mapunda alisema anawashukuru wanachama na wapenzi wa Simba kwa kumpa sapoti kwa kipindi chote alichoitumikia Simba.

“Vile vile viongozi wa Simba nao nawashukuru, japo niliitumikia vizuri kwa moyo wangu wote kwa muda wote.
Nashukuru kwa walichonifanyia kama wameona hii ndiyo njia nzuri ya kuniacha, mwisho nawatakia mafanikio mema,” alisema.

Kipa huyo wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya, St Georges ya Ethiopia na Yanga, bado aliendelea kusisitiza mipango
yake ya kurudi kucheza soka la kulipwa aliyoliambia gazeti hili Ijumaa iliyopita, hata akipata timu nyingine ya hapa hivi sasa bado amepanga kutimkia huko mipango ikienda sawa.

Hata hivyo, uongozi wa Simba kupitia kwa Mkuu wa Idara ya  Habari na Mawasiliano, Haji Manara, umesema kuachwa kwa Ivo ulikuwa ni uamuzi wa Kocha Mkuu wao, Dylan Kerr, akidai ameridhishwa na makipa walioko hivi sasa kikosini, Muivory Coast, Vincent Angban, Manyika Peter Jr na Denis Richard (Simba B).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles