25.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Ushahidi waliochoma polisi Bunju waendelea

polisNa Kulwa Mzee, Dar es Salaam

SHAHIDI wa upande wa Serikali, Abdallah Mandai, katika kesi ya kuchoma Kituo cha Polisi Bunju A amedai   kwamba aliegesha gari lake kituoni hapo aliporudi akalikuta limeharibiwa vibaya.

Shahidi huyo wa sita alidai hayo jana   mbele ya Hakimu Thimos Simba wakati akitoa ushahidi wake kwa upande wa mashtaka.

Alidai aliegesha gari hilo kituoni hapo baada ya kuona barabara imezingirwa na kundi kubwa la watu wakiwamo wanafunzi, wakiandamana.

Alidai kuwa gari hilo lilikuwa T 803 AHM Corrolla na kwamba yeye alikuwa akitokea Mbezi ya Kimara akienda  kazini kwake  eneo la Bunju kwa Baharia.

“Baada ya kuona wahuni wamejaa barabarani na hakuna sehemu ya kupita niliamua kwenda kuegesha  gari kituo cha.polisi kwani niliàmini hiyo ni sehemu salama, niliwakuta askari niliwasalimu na kuegesha gari hapo,”alidai.

Alidai  akiwa kazini kwake baada ya nusu saa alipata taarifa kwamba kituo cha polisi kimechomwa moto na alikwenda kuangalia usalama wa gari lake.

Shahidi huyo alidai akiwa njiani aliona barabara imewekwa mawe, magogo na moto uliochomwa kwa matairi ya gari na alifika katika kituo hicho cha polisi alikuta kinawaka moto.

“Gari langu lilivunjwa kioo cha mbele, nyuma, pembeni pia niliibiwa simu moja na radio ya gari,” alidai.  Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kesho

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,567FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles