26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

BASI LAGONGA TRENI, 10 WAFARIKI DUNIA

Na EDITHA KARLO-KIGOMA


WATU 10 wamefariki dunia na wengine 28 kujeruhiwa, baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugonga treni ya mizigo katika eneo la Gungu mjini Kigoma.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 12 alfajiri ikihusisha basi dogo la abiria la Hamida Safari namba  T 885 DLD, lililokuwa likifanya safari zake kati ya Kigoma na Nzega mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martine Otieno, alisema  ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa basi hilo alipotaka kuvuka reli muda mfupi baada ya kuanza safari yake kwenda Tabora.

Alisema   licha ya treni   kupiga honi, dereva wa basi hilo hakuweza kuchukua tahadhari hivyo kusababisha gari hilo kuigonga treni.

Otieno alisema baada ya treni ya mizigo kuligonga basi hilo, liliburuzwa umbali wa mita 100 kutoka eneo la ajali na kuwagonga watu wengine 17 waliokuwa wakitembea kwa miguu.

Kamanda huyo alisema uchunguzi wa awali ulibaini  chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Basi la Hamida Safari kutochukua tahadhari alipofika eneo la reli.

“Basi hili lilikuwa na   watu 20 kwa maana ya abiria 18, dereva mmoja na utingo mmoja.

“Watu waliofariki dunia papo hapo walikuwa saba, wengine wamejeruhiwa,” alisema.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma  Maweni, Dk. Osmund Ryegula alisema walipokea  maiti saba na majeruhi 28.

Alisema  wakati wakiendelea na matibabu, majeruhi wengine watatu walifariki dunia, hivyo kufanya idadi ya watu waliokufa kufikia 10.

“Tulipokea majeruhi 28 na kati ya hao wanne hali zao siyo nzuri, wameumia vibaya wapo chumba cha upasuaji wanaendelea na matibabu.

“Madaktari na wauguzi wanahangaika kuwahudumia majeruhi hao ili kuwaondoa katika hali ya hatari,” alisema.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Kapele Shaban, alisema   wakati treni ya mizigo ilipokaribia   walisikia mlio wa honi na baada ya muda mfupi wakasikia kishindo kikubwa hivyo waliamua kukimbilia eneo hilo na kukuta ajali ikiwa imetokea.

“Mimi nilikuwa mle stendi ya mabasi, nilisikia honi ya treni baadaye kishindo kikubwa kilisikika.

“Baada ya muda tulisikia taarifa za ajali na kuanza kuelekea eneo la tukio… tulianza kuwasaidia walioumia ikiwa ni pamoja na kuwatoa kwenye mabaki ya basi hilo ili kuwakimbiza hospitali,” alisema.

Athumani Julika, mkazi wa Gungu alisema alisikia treni ikipiga honi na  baada ya muda mfupi akasikia kishindo kikubwa na alipotoka nje akaona basi limeanguka.

JPM awalilia

Rais Dk. John Magufuli,  ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia vifo vya watu 10 vilivyosababishwa na ajali ya basi la abiria kugongana na treni ya mizigo Mjini Kigoma.

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilieleza kwamba Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga kufikisha salamu hizo kwa wafiwa wote, na amewaombea kuwa na moyo wa subira.

“Kwa mara nyingine tumewapoteza Watanzania wenzetu 10 katika ajali, tumepoteza wapendwa wetu na tumepoteza nguvu kazi ya Taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles