25.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

MIKOPO CHECHEFU YAATHIRI FAIDA CRDB

Eliya Mbonea, Arusha

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei amesema kutengwa kwa zaidi ya Sh Bilioni 150 kwa ajili ya mikopo chechefu kuliathiri kwa namna moja au nyingine upatikanaji wa faida wa benki hiyo.

Dk. Kimei amesema hayo leo Mei 16, mjini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akielezea kuhusu mkutano wa wanahisa wa benki hiyo utakaofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Mei 19 mwaka huu.

“Mwaka uliopita tulipata faida ya Sh bilioni 36 baada ya kukatwa kodi na kabla ya kodi tulikuwa na Sh Bilioni 53,  hii unaweza kuiona ndogo ukilinganisha na jinsi ambavyo tulikuwa tunapata awali, bado ni fedha nyingi na tunaamini katika kipindi cha mwaka huu tutapata faida zaidi.

“Kilichoathiri zaidi faida kwa miaka hii miwili iliyopita ni kulazimika kuweka tengo kubwa zaidi la mikopo ambayyo imechechefuka, CRDB tulitenga Sh bilioni 153 kwa mikopo chechefu kama tusingetenga tungepata faida ya zaidi ya Sh Bilioni 200,” amesema.

Amesema hatua hiyo ilikula kwenye faida yao na ndiyo maana faida ilipungua na kwamba benki bado inafanya vizuri pamoja licha ya changamoto nyingi zilizokuwapo ambapo hii imekuwa tofauti na matarajio.

Akielezea sababu ya kuwapo kwa changamoto hiyo Dk. Kimei amesema changamoto hiyo imetokana na mabadiliko ya kanuni za kimataifa za kutenga tengo la mikopo inayoweza kuwa chechefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles