26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

TRA YAKAMATA BIDHAA ZILIZOINGIZWA KINYEMELA ARUSHA

Eliya Mbonea, Arusha

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), imekamata mifuko ya sukari 362, galoni 100 za mafuta ya kula ya Nyota na maboksi 40 ya Karibu, yakidaiwa kuingizwa nchini bila kulipiwa ushuru katika maeneo ya Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Akizungumza mjini hapa jana Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema, bidhaa zote zilizokamatwa zina thamani ya zaidi ya Sh milioni 20 huku kodi ya bidhaa hizo ikiwa ni Sh milioni 28.5 huku adhabu kwa bidhaa zote ikiwa ni Sh milioni 10.7.

Amesema usiku wa kuamkia Mei 11, mwaka huu malori mawili yenye namba T985AJP na T840ABF yalikamatwa yakiwa yamepakia bidhaa hizo za magendo ambapo mara baada ya kukamatwa yalihifadhiwa ofisi za TRA wilayani Ngorongoro.

“Jumla ya mapato yanayotakiwa kulipwa serikalini ni Sh milioni 39.2, wafanyabiashara hawa wamevunja kifungu cha Sheria namba 200 na 82 ya Sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 na Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2005,” amesema.

Amesema kulingana na sheria hizo wafanyabiashara hao wanatakiwa kulipa faini huku magari na bidhaa zilizokamatwa zikitaifishwa na serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles