26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

BUNGE LAIKOMALIA SERIKALI KODI YA TENDE

Gabriel Mushi, Dodoma

Bunge limeendelea kuibana Serikali itekeleze agizo la kuondoa kodi kwenye tende ili kuwawezesha waumini wa dini ya kiislamu kupata bidhaa hiyo kwa urahisi katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni jijini Dodoma na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson wakati akitolea ufafanuzi mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali.

Bobali aliliomba Bunge kujadili hoja hiyo kwa muda wa dakika 30 kwa kuwa licha ya wabunge kadhaa akiwamo Mbunge wa Ubungo, Saed Kubene (Chadema) na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), kuiomba serikali iondoe kodi kwenye tenda katika vikao vilivyopita, bado serikali haijatekeleza.

Amesema tende katika nchi za Kenya, Zanzibar na Msumbiji zimefutiwa kodi lakini inashangaza kwa upande wa Tanzania bado haijafutiwa kodi.

“Sasa mwezi wa Ramadhani unaanza wiki ijayo na makontena yapo kwenye meli bandarini ambayo yametolewa kwa msaada wa mali za wakfu, watu wanajichangisha mali za wakfu zinaletwa na wao wanatafuta thawabu. Sasa naliomba Bunge walau nusu saa, kwa sababu jambo hili linaiaibisha Tanzania,” amesema.

Akitolea ufafanuzi huo Dk. Tulia alisema kwa kuwa jambo hilo limeshazungumzwa na utaratibu wake upo kisheria, serikali haina wajibu wa kutekeleza.

“Nadhani serikali ifanyie kazi jambo hili ione namna bora ya kushughulikia, kama ambavyo Bobali ametaja mifano ya huko kwingine sijasoma sheria zao.

“Lakini sheria tunatunga wabunge, ila watekelezaji serikali, upande wa watekelezaji muangalie namna ya kushughulikia jambo hili ili mwezi wa Ramadhani unapokuja wenzetu wenye imani ya kiislamu  waweze kupata hizo huduma ambazo zipo kiutaratibu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles