25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAPATA TABU KUKIRI NJAA

Gabriel Mushi, Dodoma

Serikali imesema inapata tabu kukiri kuwa kuna hali ya njaa nchini kwa kuwa mvua zimenyesha za kutosha mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 2, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu (CCM), Khadija Nasri Ally.

Mbunge huyo alitaka kujua kauli ya serikali kuhusu hali ya njaa na umaskini nchini.

Alisema ripoti za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Taasisi ya utafiti (REPOA), zimebainisha kuwa hali ya njaa na umaskini imeongezeka mwaka huu ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Akijibu swali hilo Dk. Kijaji amesema hali ya njaa nchini haipo kwani mvua za kutosha zimenyesha na wananchi wana amani kwani hakuna uhaba wa chakula.

“Napata tabu kusema kusema hali ya njaa imeongezeka ndani ya mwaka 2018 wakati mfumuko wa bei za bidhaa zinazochangia upatikanaji wa chakula nchini kwa mwezi Machi mwaka huu ulikuwa asilimia 3.9 pekee.

“Hii ni dalili kuwa hali ya njaa nchini haipo labda mbunge ametumia takwimu za miaka iliyopita mwaka 2016/17 ,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles