26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MAJALIWA ATAMANI KUWA KAMA SOKOINE

Na ELIYA MBONEA-MONDULI


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema  anamuomba Mwenyezi Mungu amuongoze kufanya na kutenda kama alivyokuwa Edward Moringe Sokoine wakati wa uongozi wake.

Hayo alisema wilayani Monduli mkoani Arusha jana wakati wa Ibada ya kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 34 ya kifo cha Hayati Sokoine yaliyofanyika nyumbani kwake kijijini Monduli Juu.

Majaliwa ambaye kwa sasa ni Waziri Mkuu wa Nane tangu Hayati Sokoine, alisema kiongozi huyo alikuwa mahiri na mtu msikivu katika kulitumikia taifa.

“Sokoine hakuwa na ubinafsi wala kinyongo na mtu yeyote, kubwa zaidi hakuwa na tamaa ya mali wala madaraka.

“Kuna jambo la kujifunza kwetu sisi watumishi wa umma kuendelea kuenzi mchango wake na hasa mimi niliyepo kwenye nafasi aliyokuwa akiongoza.

“Namuomba Mungu aniongoze kufanya na kutenda kama Edward Sokoine,”  alisema.

Alisema katika kuhakikisha wanafuata nyayo za hayati Sokoine  aliyekuwa akikemea wala rushwa na walanguzi, leo Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikijitahidi kutembea katika dira aliyoisisitiza Sokoine.

“Serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk.John Magufuli imekuwa mstari wa mbele kutembea kwenye maono na dira ya Sokoine.

“Imeweza kupambana na wala rushwa, mafisadi, watumishi hewa, dawa za kulevya na kuhakikalikisha maadili ndani ya utumishi wa umma yanazingatiwa,” alisema Majaliwa

Awali akiongoza Ibada Askofu Mkuu mstaafu Josaphat Lebulu,  aliwataka viongozi na Watanzania kuhakikisha wanaitunza amani ya nchi kuendelea kuifanyaTanzania kuwa maskani mazuri ya kuishi.

Alisema kumbukumbu ya hayati Sokoine huwazamisha katika kukumbuka utumishi na uwajibikaji uliotukuka.

“Ndugu zangu viongozi na wananchi, tuwe waaminifu kwa nchi yetu, tuitunze na kuifanya kuwa maskani mazuri ya kuishi.

“Ni aibu kwa Mtanzania kumkuta akiitukana nchi yake, utaskia mtu anasema watu wa hapa ni bure, tuipende nchi yetu kama Sokoine alivyotufudisha,” alisema Askofu Lebulu

Waziri wa Katika na Sheria, Professa Palamagamba Kabudi, alisema katika maisha ya binadamu duniani wapo watu ambao huwa hawafai.

“Nyerere amekataa kufa na Sokoine amegoma kufa, kila siku watu hawa wanaishi hivyo tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwao. Sokoine katika uongozi wake alijiongeza,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles