24.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

MPAMBE WA RAIS APANDISHWA CHEO

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


RAIS Dk. John Magufuli amempandisha cheo Luteni Kanali, Bernard Mlunga kuwa Kanali na ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais (Aide de Camp – ADC).

Kanali Mlunga ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Kanali Mbaraka Mkeremy ambaye amepandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali.

Taarifa  jana na Kurugenzi ya Mawasiliano  ya Rais, Ikulu na kusomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, imeeleza kuwa Rais Dk. John Magufuli, amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika vyeo mbalimbali.

Rais amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Massao kuwa Luteni Jenerali. Meja Jenerali Massao ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya maofisa Wanafunzi wa Jeshi Monduli (TMA) na kwa uteuzi huo, sasa JWTZ itakuwa na Luteni Jenerali wawili.

Rais Magufuli pia amempandisha cheo Brigedia Jenerali Henry Kamunde kuwa Meja Jenerali.

Vilevile amewapandisha vyeo maofisa 27 wa JWTZ kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali na ofisa mmoja kutoka Luteni Kanali na kuwa Kanali.

Waliopandishwa vyeo hivyo ni D. D. M Mullugu, J. J Mwaseba, A. S Mwamy, R. K Kapinda, C. D Katenga, Z. S Kiwenge, M. A Mgambo, A. M Alphonce, A. P Mutta, A. V Chakila, M. G Mhagama, V. M Kisiri, C. E Msolla na S. M Mzee.

Wengine ni C. J Ndiege, I. M Mhona, R. C Ng’umbi, S. J Mnkande, A. C Sibuti, M. M Mumanga, I. S Ismail, M. N Mkeremy, G. S Mhidze, M. A Machanga, S. B Gwaya, P. K Simuli na M. E Gaguti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles