29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

‘VIONGOZI WA DINI HIMIZENI JAMII CHANJO YA SARATANI’

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Serikali imewaomba viongozi wa dini kuhamasisha jamii kuhusu chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya saratani ya kizazi (HPV).

Rai hiyo imetolewa leo Ijumaa Aprili 6, na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika kikao chake na viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini jijini Dar es Salaam.

“Chanjo hii haihusiani kabisa na masuala ya uzazi wa mpango (nyota ya kijani), na imethibitishwa kwamba ni salama kwa afya, hii ni kinga dhidi ya saratani ya kizazi, lengo letu ni kuwakinga wasichana kwani takwimu zinaonesha inaongoza kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa.

“Takwimu za Taasisi ya Saratani Ocean Road zinaonesha saratani ya shingo ya kizazi inaongoza kwa asilimia 32 hadi 34 kwa mwaka, ikifuatiwa na saratani ya matiti kwa asilimia 12 huku saratani ya tezidume kwa asilimia mbili,” amesema.

Amesema serikali tayari imepokea chanjo hiyo na kwamba itazinduliwa rasmi April 10, mwaka huu na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika kikao hicho, Sheikh Yusuph Tungi ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Bakwata amesema wako tayari kushirikishana na serikali kufikia ujumbe huo kwa jamii.

Naye Askofu wa Kanisa la Adventista Wasabato, Jimbo la Kusini Mashariki mwa Tanzania, Steven Ngussa ameishauri Wizara kutumia pia mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe kuhusu magonjwa mbalimbali ikiwamo hayo ya saratani.

MWISHO

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles