32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kinana: Serikali irahisishe upatikanaji leseni wilayani

KINANAANa Patricia Kimelemeta, Ngara
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, ameitaka Serikali kurahisisha upatikanaji wa leseni kwenye wilaya zote nchini badala ya kutolewa makao makuu ya miji pekee.
Alisema kufanya hivyo ni kuchelewesha maendeleo na shughuli za Watanzania ambao wanajitafutia riziki na badala yake mchakato huo uwafuate wananchi kwenye wilaya zao.
Kinana alitoa wito huo jana wakati akihutubia wananchi wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, katika ziara yake ya siku 10 ya kujenga na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na uhai wa chama mikoani.
Alisema leseni za vyombo vya moto pamoja na leseni za kuendesha pikipiki zinatakiwa kutolewa kwenye wilaya ili kupunguza gharama za ufuatiliaji na muda.
“Hivi inawezekana vipi mtu ananunua pikipiki ya shilingi milioni moja, anatakiwa kwenda makao makuu ya mji kusajili, anatumia muda na fedha nyingi kutafuta usajili kazi ambayo inaweza kufanyika kwenye kila wilaya, hii siyo sawa tunapaswa kujadili mfumo huu huku ni kuwatesa wananchi na kuwacheleweshea shughuli zao za maendeleo,” alisema Kinana.
Alisema kutokana na uzito wa suala hilo, alihaidi kulifikisha katika vikao vya Kamati Kuu (CC), pamoja kwa Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta kama njia ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu.
Pamoja na hilo, Kinana alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella, kuhakikisha anafuatilia suala hilo katika ngazi ya mkoa ili hatua ziweze kuanza kuchukuliwa kwa masilahi ya wananchi.
“Katibu Mkuu wa CCM, tumekuwa tukifuata leseni makao makuu ya mji wa Bukoba, tunatumia zaidi ya wiki kufuatilia lakini unaweza kurudi bila leseni, hili linatupa shida tunaomba Serikali itusaidie,” alisema Johnson Mkibika mkazi wa Kijiji cha Bamako.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles