26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tiper yasaidia vifaa vya maabara Shule ya Msafiri

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya kuhifadhi mafuta nchini, Tiper imetoa msaada wa vifaa vya maabara vyenye thamani ya Sh milioni 20 kwa Shule ya Sekondari Msafiri, iliyopo wilayani Rufiji, mkoani Pwani ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za kampuni hiyo katika kuboresha kiwango cha elimu nchini.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika jana wilayani Rufiji, Mkurugenzi Mtendaji wa Tiper, Daniel Belair, alisema msaada huo pia ni sehemu ya mpango endelevu wa kampuni hiyo katika kusaidia jamii.
“Tiper tunaamini katika kuwekeza kwenye jamii inayotuzunguka na taifa kwa ujumla hususani katika suala zima la elimu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, uwekezaji kwenye elimu ya vijana wetu hasa kwenye sayansi ndiyo maandalizi ya kesho tunayoihitaji,’’ alisema.
Belair aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wanavitumia vifaa hivyo sambamba na kuwa makini na utunzaji kwa manufaa yao.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Diwani wa Kata ya Bungu, Ramadhani Mkwaya (CCM), alisema: “Napenda kuwashukuru Tiper kwa msaada wao huu unaolenga pia kuunga mkono mpango wa Serikali wa ‘Matokeo Makubwa sasa”, alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo, Maulid Mwita, aliuhakikishia uongozi wa Tiper kuwa wao kama walimu wa shule hiyo watahakikisha malengo ya kukabidhiwa vifaa hivyo yanakamilika kwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi wao hasa kwenye masomo ya sayansi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles