27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya Exim yaaadhimisha siku ya damu duniani

Na Adam Mkwepu, Dar es Salaam
WAFANYAKAZI wa Benki ya Exim Tanzania, wameadhimisha siku ya kuchangia damu duniani.
Kutokana na uzito wa siku hiyo, mwishoni mwa wiki walijitokeza makao makuu ya benki ya damu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku hiyo, kama njia ya kutambua umuhimu wa hitaji hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati zoezi hilo likiendelea, Mkuu wa Kitengo cha rasilimali watu wa benki hiyo, Frederick Kanga, alisema hatua hiyo ni mwendelezo tu kwa kuwa wafanyakazi hao wamekuwa wakifanya hivyo tangu mwaka 2010 na lengo kuu ni kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu salama kwenye vituo vya afya hapa nchini.
“Mara zote tumekuwa tukijisikia kuwa na furaha ya ajabu inapofika siku kama hii kwa kuwa tunaamini kwamba tunapata fursa ya kutimiza wajibu wetu kama sehemu ya jamii, lakini pia kwa kufanya hivyo tunakuwa tumeshiriki kuokoa maisha ya wenzetu wanaopoteza maisha kwa kukosa damu salama pale wanapoihitaji,” alisema Kanga.
Kauli hiyo inakwenda sambamba na kauli mbiu ya uchangiaji damu ya mwaka huu inayosema: ‘Asante kwa kuokoa maisha yangu’, ambayo inalenga kuwashukuru wote wanaochangia damu na hivyo kuokoa maisha ya wenzao kila siku huku ikiwahamasisha watu ulimwenguni kote kuchangia damu kila wakati.
Akizungumza wakati akisimamia zoezi hilo, Ofisa Uhamasishaji na Elimu kwa Umma wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), Lucas Michael, alisema uhaba wa damu nchini umekuwa ukichangiwa kwa kiasi kikubwa na mtazamo wa wananchi walio wengi kwamba wapo tayari kuchangia damu pale tu inapohitajiwa na mmoja wa wanandugu wa familia husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles