Na Leonard Mang’oha, Dar es Salaam
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameitaka serikali ya Japan kuboresha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hiyo na Tanzania ili kusaidia kukuza uchumi na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika jamii.
Ameyasema hayo leo wakati wa kusaini mikataba mitano ya miradi ya maendeleo yenye thamani ya Sh milioni 991 itakayotekelezwa katika halmashauri tano za mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Halmashauri ya Kigoma.
Zitto amesema pamoja na misaada mbalimbali inayotolewa Tanzania haitaweza kupiga hatua kwa kuomba misaada ya madarasa na miradi mingine bali kunahitajika kuimarishwa kwa ushirikiano wa kibiashara baina nchi hizo.
Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida amezitaka halmashauri hizo kuhakikisha zinatekeleza miradi hiyo kwa kama walivyokubaliana na kwa wakati.