31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA YARUHUSU BABU SEYA KUDAI FIDIA

 

Na Eliya Mboneya, Arusha

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu(AfCHPR), imesema Mahakama za ndani Tanzania katika kesi ya kubaka na kulawiti iliyokuwa inamkabili mwanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na mwanawe Johnson Nguza (Papii Kocha) zilitenda haki kwa kiwango kikubwa na kwa upande mwingine zilikiukwa.

Aidha, kutokana na kukiukwa kwa baadhi ya haki zao hizo, mahakama hiyo imewaruhusu kuwasilisha hoja na kuainisha ni namna wanaweza kuomba fidia kulingana na haki zao ziliokiukwa ndani ya siku 30 huku upande wa Jamhuri ukitakiwa kujibu hoja hizo ndani ya siku 30.

Akitoa hukumu hiyo katika mahakama hiyo leo Ijumaa Machi 23, Kiongozi wa majaji nane waliokuwa wakisilikiza shauri hilo, Gerald Niyungeko mbele ya Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Sylvain Ore, amesema baadhi ya haki zilizotendwa ni pamoja na kuwaachia watuhumiwa watatu kwenye kesi hiyo pamoja na kubakiza mashitaka manne kati ya 21 yaliyokuwa yakiwakabili.

“Haki zao hazikukiukwa kulingana na uamuzi uliotolewa na mahakama za ndani za Tanzania kwa kuwaachia washtakiwa wengine na kupunguza mashtaka 21 hadi manne, lakini kwa upande mwingine zilikiukwa, kwa mfano wakiwa Mahakama ya Halimu Mkazi Kisuti walikaaa mahabusu kwa siku nne bila kufahamishwa makosa yao lakini pia hawakuwa na wakili wa kuwatetea.

“Aidha, waleta maombi pia waliomba kupimwa mkojo na damu ili kuthibitishwa kama waliwaingilia wale watoto ambao upande wa jamhuri ulidai waliambukizwa magonjwa ya zinaa lakini walikataliwa.

“Kwa upande mwingine, Nguza aliomba kupimwa kama ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa au lakini pia alikataliwa,” amesema Jaji Niyungeko.

Hata hivyo, kuhusu kupinga kifungo cha maisha, Jaji Niyungeko amesema mahakama haikujielekeza katika shauri hilo kwa sababu waleta maombi wako huru kwa msamaha wa rais hivyo haikuona sababu ya kushughulikia hilo kwani wako nje kwa mujibu wa sheria.

Babu Seya na Papii Kocha waliachiwa kwa msamaha wa rais Desemba 9, mwaka jana kutokana na kifungo cha maisha jela walichohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Juni mwaka 2004 baada ya kumkuta na hatia ya kunajisi na kulawiti watoto 10 ambapo walikata rufaa Mahakama za juu na kugonga mwamba na hivyo kulazimika kukimbilia AfCHPR wakidai haki zao zilivunjwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles