27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

OBASANJO: BOKO HARAM NI MATOKEO YA KUKOSA ELIMU, AJIRA

Na Arodia Peter, Kigali

Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo amesema vijana wengi wanajiunga na kundi la kigaidi la Boko Haram kutokana na kukosa ajira na elimu.

Akizungumza kwenye mjadala wa Wataalamu wa Uchumi jijini Kigali, Rwanda leo Jumanne Machi 20, kuhusu kulifanya bara la Afrika kuwa eneo moja huru kibiashara Obasanjo amewataka viongozi wa Afrika kuhakikisha suala la elimu na ajira kwa vijana linapewa kipaumbele ili kuziondoa nchi hizo kuwa makazi ya makundi hatari kwa ustawi wa Afrika.

Katika hatua nyingine, Rais huyo Mstaafu wa Nigeria amempongeza Rais mpya wa Zimbabwe, Emmarson Mnangagwa kwa kazi kubwa iliyofanywa na Wazimbabwe kupita salama katika kipindi alichokiita cha mpito.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles