23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

UINGEREZA YAFUKUZA WANADIPLOMASIA 23, URUSI NAYO KULIPA KISASI

LONDON, UINGEREZA


WAZIRI Mkuu wa Uingereza Theresa May ametangaza kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa nchi hiyo, kusitisha mawasiliano ya kiserikali na kufuta mwaliko kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov.

Hatua ya Uingereza ni jibu la shambulio dhidi ya aliyekuwa jasusi wa Urusi nchini humo Sergei Skripal, Urusi imesema kuwa hatua za Uingereza dhidi yake ni za uhasama na zilizochukuliwa kwa pupa na kwamba itajibu mapigo.

May ameliambia Bunge la Uingereza kuwa jaribio la mauaji dhidi ya Skripal na bintiye Yulia katika mji wa Salisbury unawakilisha matumizi ya Urusi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya Uingereza.

May alisema kuwa baada ya tukio hilo la kushangaza, uhusiano wa taifa lake na Urusi huwezi kusalia kama ulivyokuwa awali.

Ameongeza kusema, kwa hivyo tutasitisha mawasiliano yoyote yaliyopangwa kati ya Uingereza na Urusi.

Hii ni pamoja na kufutilia mbali ziara ya Lavrov, pia familia ya kifalme na wanasiasa hawatahudhuria kombe la Dunia litakaloandaliwa Urusi baadaye mwaka huu.

Ametangaza hatua hizo baada ya Urusi kupuuza muda wa mwisho uliotolewa kueleza kuhusu sumu iliyotengenezwa zama za Umoja wa Kisovieti wa Urusi ilivyotumika dhidi ya Sergei na Yulia Skripal.

Lakini Ikulu ya Urusi imesema hatua za kulipa kisasi zitakuja muda si mrefu huku Rais Vladimir Putin akitarajia kuchagua njia ambazo zitakuwa na maslahi zaidi ya Urusi.

Lavrov alilaani madai kuwa Urusi iko nyuma ya njama za kumuua Skripal huko Salisbury Machi 4 kuwa tuhuma za kipuuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles