22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MHUDUMU AANGUKA KUTOKA KWENYE NDEGE UGANDA

KAMPALA, UGANDA


MHUDUMU wa ndege anadaiwa kujeruhiwa vibaya nchini hapa baada ya kuanguka kutoka mlango wa dharura wa ndege ya Shirika la Emirates juzi Jumatano.

Mwanamke huyo alikimbizwa hospitali akitokea uwanja wa ndege wa kimataifa Entebbe, karibu na hapa.

Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilitua muda mfupi kabla na ilikuwa ikijiandaa kupokea abiria kabla ya kuelekea Dubai.

Mazingira ya kuanguka kwake yanaendelea kuchunguzwa, huku kukiwa na ripoti za kukanganya kuhusu tukio hilo ikiwamo za kujirusha.

Hata hivyo, shirika hilo limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

“Tunaweza kuthibitisha kuwa mmoja wa wafanyakazi wetu bahati mbaya alianguka kwenye mlango uliokuwa wazi wakati alipokuwa akiiandaa ndege ili kupandisha abiria.”

“Mfanyakazi huyo amepelekwa kwenye hospitali ya karibu. Tunatoa ushirikiano kadiri iwezekanavyo kwa mfanyakazi wetu, na kutoa ushirikiano zaidi kwa mamlaka zinazofanya uchunguzi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles