25.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

EFD yapunguza mapato ya serikali

mkuyaWAZIRI wa Fedha, Saada Mkuya, amesema mwitikio mdogo wa wafanyabiashara katika utumiaji wa mashine za kielektroniki (EFD) ni moja ya sababu za kutofikia lengo la makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha unaoisha.
Akiwasilisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/16 mjini Dodoma jana, Waziri Saada alisema hadi Aprili mwaka huu mapato ya kodi yalikuwa yamefikia Sh trilioni 8.1 sawa na asilimia 72 ya makadirio ya mwaka ya Sh trilioni 11.3.
Waziri Saada alisema sababu nyingine ni pamoja na kushuka kwa makusanyo yatokanayo na shughuli za utafiti na uchimbaji wa gesi, mafuta na madini, hususan kodi ya zuio.
Alitaja pia makusanyo hafifu kutoka kwenye ushuru wa bidhaa za vinywaji baridi, sigara, bia na tozo za huduma za kibenki pamoja na kupungua kwa ukuaji wa uagizaji wa bidhaa zisizo za kimtaji.
Hata hivyo, alisema pamoja na changamoto hizo, inakadiriwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu mapato ya kodi yatafikia asilimia 91 ya lengo la mwaka.
Kwa upande wa mapato yasiyo ya kodi, alisema hadi kufikia Aprili, mwaka huu yalifikia Sh bilioni 534.4 ikiwa ni sawa na asilimia 62 ya lengo la kukusanya Sh bilioni 859.9 kwa mwaka na kwamba inakadiriwa hadi mwishoni mwa mwezi huu mapato yasiyo ya kodi yatafikia asilimia 74 ya lengo la mwaka.
Hata hivyo, alisema Serikali imejitahidi kupunguza misamaha ya kodi ambapo hadi Aprili mwaka huu ilifikia kiasi cha sh bilioni 1.3 sawa na asilimia 1.4 ya pato la taifa na hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu inatarajiwa kufikia Sh bilioni 1.4 sawa na asilimia 1.5 ya pato la taifa ikilinganishwa na misamaha ya kodi ya sawa na asilimia 2.0 ya pato la taifa iliyotolewa mwaka 2013/14.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles