NA AZIZA MASOUD
MTANDAO wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), umerekodi wimbo maalumu wa elimu juu ya uhamasishaji wa utunzaji na kuzuia uharibifu wa misitu.
Wimbo huo umeimbwa na wasanii; Mrisho Mpoto, Suleiman Msindi (Afande Sele) na Dyna Nyange, huku maudhui yake yakilenga elimu ya utunzaji wa misitu kutokana na umuhimu wake kwa jamii.
Akizindua wimbo huo pamoja na video yake, mjumbe wa Kikosi cha Taifa cha Mkulumi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Julita Masanja, alisema kupitia wimbo huo jamii itapata ujumbe kwa haraka tofauti na kuandikwa kwenye vitabu.
“Watu wengi wanapenda kusikiliza na kuona kuliko kusoma, hivyo wimbo huu ni njia mwafaka ya kuwafikishia wananchi ujumbe kwa ufasaha,” alisema Masanja.