UUZAJI bikira kwa sasa umekuwa dili zuri linalovutia wasichana na wanawake wengi wenye umri mdogo barani Ulaya na Asia.
Biashara hii huwaingizia wahusika fedha nyingi na za haraka na kuzitumia katika mambo mbalimbali yakiwamo ya kimaendeleo kama vile ununuzi wa nyumba, mtaji wa biashara, kujiendeleza na hata kuuguza.
Miongoni mwa mataifa ambayo biashara hii imeshamiri ni pamoja na Urusi, ambako wasichana na wanawake hutunza bikra zao hadi wafikishapo umri unaokubalika kisheria kisha kuziuza kwa wanaume matajiri barani Ulaya na Asia.
Hata hivyo, wasichana na wanawake wengine wengi wao si wa kweli, kutokana na tamaa hufanyiwa upasuaji ili kurudisha bikra zao kisha kuendelea na biashara hiyo tena na tena hadi mara 15.
Mitandao ya wafanyabiashara na maskauti katika mitandao ya kompyuta imekuwa ikihamasisha na kuvutia wasichana na wanawake bikra, ambao hufikia makubaliano ya kuunganishwa na wafanyabiashara matajiri.
Mawakala au tuseme makuwadi hawa hufaidika na sehemu ya tozo la ada, ambazo huanzia kati ya mamia hadi makumi kwa maelfu ya dola kutegemea na na umri au urembo wa msichana husika.
Katika kesi nyingine, wanawake huweka matangazo wakiuza haki ya kuutumia nao usiku mmoja katika majukwaa na tovuti za uchumba mitandaoni ili kuvuta wanaume mashuhuri na wenye fedha.
Moja ya matangazo kutoka jukwaa la “Bad girls club” linaeleza: “Tunatafuta wasichana wa kila aina walio bikra chini ya umri wa miaka 19, nadhifu, warembo, wachangamfu kutoka majiji yoyote ya Urusi. Tunawalipia tiketi kwenda Moscow na kurudi siku moja au mbili, aina ya wasichana ni kama hawa uwaonao pichani.”
Mtandao mwingine wa kijamii nchini Urusi unaotafuta wasichana na wanawake wadogo ni ‘Desperate Virgins Club.’
Msichana mwenye umri wa miaka 19 kutoka Moscow, akijiita Milana Mercer, anasomeka katika tangazo maalumu la mtandaoni: “Kuuza bikira, tafadhali nitumie ujumbe wa maneno. Natokea Moscow, nina miaka 19 urefu wa futi 5’9” na uzito wa pauni 143.”
Ujumbe mwingine unaotangaza uuzaji na ununuzi wa bikra, unajinasibu: “Usokose fursa hii. Marina aliuza bikira yake Sh milioni 70 na kununua bonge la mjengo.”
Msichana mwingine Anastasia (20) kutoka jiji la viwanda la Magnitogorsk aliiambia Bumaga, tovuti ya mitindo kuwa kwa sasa anatoa ofa ya kuuza bikira yake kupata fedha za matibabu ya saratani kwa ajili ya mama yake. Anasubiri ofa ya Sh milioni 16 kwa mujibu wa ripoti.
“Badala ya kupoteza ubikira wangu hivi hivi, ni bora niitumie kwa kutengeneza fedha,” anasema Lena (18) wa Moscow.
“Huu si ukahaba, nataka kukutana na mwanamume tajiri na kujaribu uhusiano naye,” anaeleza msichana mwingine Dasha (19).
Naye Rita (18) anayetoka mji wa Rostov, anasema: “Ili kuanza biashara, unahitaji mtaji. Huwezi kupata fedha nyingi kwa kazi za kawaida, lakini hapa huhitaji kufanya chochote, ni bikra yako tu.”
Mmoja wa wateja, Dmitry (38) kutoka Siberia, anasema mara mbili alinunua bikra ya wasichana wa miaka 18, akilenga kuchukua jumla, yaani kuoa mwanamke ambaye hajawahi kukutana na mwanamume mwingine.
Mara ya kwanza hilo ilimgharimu Sh milioni nne na wa pili Sh milioni tatu lakini alishindwa kumpata mke anayemtaka.
Marina ambaye aliuza bikra yake pamoja na kufanyiwa upasuaji mara kwa mara kwa kipindi cha miaka saba kabla ya kuacha kutokana na umri, kwa sasa ni meneja akiendesha mtandao unaounganisha wasichana wadogo kwa wateja matajiri.
Ijapokuwa bei ya kununua bikra nchini humo inafikia hadi Sh milioni 100, mara nyingi ili kupata wateja mara kwa mara huwa ni kati ya Sh milioni nane hadi 17, ambapo malipo hutegemeana na umri na mwonekano.
Hata hivyo, bikra huweza kuuza hadi Sh bilioni sita kwa njia za mnada. Kwa mfano; mwanafunzi Catarina Migliorini wa nchini Brazil aliiuza bikira yake kwa Sh bilioni mbili kwa tajiri mmoja wa Australia.
Mwingine Aleexandra Kefren (18) wa Romania baada ya mnada aliuza bikra yake kwa bilionea mmoja wa Hong Kong kwa Sh bilioni sita huku sehemu ya fedha hizo akiweka ahadi ya kuwanunulia nyumba wazazi wake.
Wasichana wanaopendwa zaidi ni wenye umri wa miaka 17 na 18 wafupi na wenye mvuto wa kimapenzi na wenye unyenyekevu.”
Kwa wastani mameneja huuza hadi wasichana 10 bikra kwa mwezi na kujipatia kipato cha Sh milioni 18 kwa mwezi.
Wale wauzao ubikra hupaswa kuonesha vyeti vya hospitali kuthibitisha kuwa hawajawahi kufanya mapenzi.
Lakini wanawake wengi hupitia upasuaji kurudisha ubikira kisha kuwalaghai wanaume wakiamini bado ni bikra na kuendelea kujipatia fedha katika soko hilo lenye faida. Hii ni kwa muijibu wa ripoti ya Bumaga.
Mwaka 2016 mwanamitindo Anna Feschenko (17) alielekea Dubai akilenga kuuza ubikra wake kwa dola Sh milioni 30 kwa mwanamume tajiri wa Kiarabu.
Lakini mama wa Feschenko aliwatonya polisi na msichana huyo akarudi kutoka Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE). Hata hivyo, haikujulikana iwapo aliuza ubikra au la, baada ya kugoma kuzungumzia hilo.
Katika kesi nyingine, mama mwingine alikamatwa kwa kujaribu kumuuza binti yake bikra (13) kwa mteja tajiri.
Mama huyo Irina Gladkikh (35) alisafiri kwenda Moscow kutoka Chelyabinsk ili kuuza bikra ya bintiye mwenye umri mdogo kwa mfanyabiashara tajiri kwa Sh milioni 60.
Mwisho.