26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

ATUMIA PICHA YA MCHEZA FILAMU ZA NGONO ‘KUFUKUZA WACHAWI’ SHAMBANI

JOSEPH HIZA NA MASHIRIKA


MKULIMA nchini India ameweka shambani kwake bango kubwa la mcheza filamu maarufu za ngono nchini humo ili kulinda mazao yake.

Mkulima huyo, Chenchu Reddy (45), anasema mbinu yake hiyo mbadala imefanya kazi na anaamini picha hiyo ina uchawi wa kutosha kusaidia na kulinda mazao yake.

Reddy hulima mazao katika shamba lake hilo lenye ukubwa wa ekali 10 katika jimbo la Andhra Pradesh, na anasema kustawi kwa mazao kumevuta kijicho cha husuda kutoka kwa wanakijiji na wapita njia.

Hivyo, bango hilo la mcheza filamu maarufu Sunny Leone hukimbiza ‘jicho baya’.

Bango hilo linasomeka: “Hey, usilie au kujisikia wivu kwa ajili yangu!” na lina picha ya mcheza filamu huyo za ngono akiwa amepozi na bikini nyekundu.

Akizungumza na gazeti la Hindustan Times la humo, mkulima huyo mwenye imani za kishirikina anasema utumiaji wake wa ‘nguvu ya mvuto wa matiti’ umefanya kazi vyema.

Hakuna mtu anayeangalia tena mazao yangu ya koliflawa na kabichi bali macho yote huelekezwa sasa kwa msichana mrembo mwenye mvuto.

Anasema: “Mwaka baada ya mwaka, nimekuwa nikipata hasara kwa kuvuna mazao kiduchu na dhaifu.

“Mazao yalionekana yenye afya kwa muda kisha mambo yakabadilika kuelekea kunyauka.

“Mwaka huu nimepata mazao mazuri katika eka 10. Hili kwa kawaida huvuta macho ya wanakijiji na wapita njia,” anasema.

Anaongeza: “Kuondoa macho ya kichawi, niliwazia wazo hili la kuweka picha kubwa ya Sunny Leone siku chache zilizopita.

“Mbinu imefanya kazi, kwani hakuna mtu anayeangalia tena mazao yangu bali macho huelekezwa katika msichana huyo mwenye mvuto.”

Njia nyingine zinazotumiwa kulinda mazao ni pamoja na kuweka midoli wabaya au sahani za chuma zenye picha za mapepo.

Kuhusu uwezekano wa kibano kutoka mamlaka husika kwa kutumia mbinu hizo, anasema: “Maofisa kamwe hawana muda wa kuja huku mashambani kwetu kutatua matatizo na hivyo sidhani kama kinga hizi zinasumbua.”

Mwisho

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles