29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

WAISLAMU NCHINI WATAKIWA KUSHIKAMANA

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

 

Balosi wa Iran, nchini Tanzania, Mousa Farhang, amewataka Waislamu kuwa na mshikamano na umoja ili kujenga umma wenye mapenzi mema na kuondoa hofu miongoni mwao iliyojengwa ili kuuangamiza Uislamu na kuondoa dhana ya Uislamu ni ugaidi.

Akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa uliohusisha wanazuoni na maimamu kutoka nchi mbalimbali Dar es Salaam leo Alhamisi Februari 22, Balozi Farhang amesema umefika wakati sasa Waislamu kukaa meza moja, kujadiliana na kuzungumza masuala ya kujenga ili kupambana na wanaojaribu kujenga hofu kwamba Uislamu ni ugaidi.

“Lazima Waislamu tushikamane pamoja na tuwe umma wenye mapenzi mema, imefika wakati sasa Waislamu tukae pamoja katika kujadiliana, kuzungumza masuala ya kujenga kuangalia wapi kuna tatizo kwenye kujenga Uislamu,” amesema.

Aidha, amesema katika zama hizi damu ya Waislamu ni rahisi sana kumwagwa na kuna Waislamu wanawake wanauzwa kama bidhaa ambapo hayo yanaweza kumalizika kwa Waislamu kuungana pamoja kukaa katika meza ya majadiliano, mazungumzo kwa kuwa kuna maadui wanaojaribu kuungamiza Uislamu kwa kujenga hofu kwamba Uislamu ni ugaidi.

“Umefika wakati tupambane na watu hawa tukae kuzungumza katika meza moja kumaliza tatizo hili,” amesema.

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, amesema mkutano huo wa kimataifa umewaleta waislamu pamoja bila kujali madhehebu.

“Umadhehebu usipoteze umoja baina ya Waislamu, wakati tulionao lazima tushikamane kama Waislamu mkono kwa mkono kwa kuwa hakuna sababu ya kutengeneza utofauti wa madhehebu,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles