22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

PROFESA NDALICHAKO AKARIBISHWA KWA MABANGO AQUILINA AKIAGWA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amekaribishwa kwa mabango na wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakati akipanda jukwaani kutoa hotuba yake katika shughuli ya kutoa heshima ya mwisho kwa Aquilina Akwilini.

Baadhi ya mabango hayo yalikuwa yanasomeka ‘We are tired of being killed’, ‘Mwigulu, Siro kwa mauaji haya bado mpo Ofisini?’na ‘Wauaji hawawezi kujichunguza’.

Baada ya kupanda jukwaani, Profesa Ndalichako amesema serikali inachukulia suala hili kwa uzito na Rais ameshaagiza wahusika wanachukuliwa hatua.

“Mimi natoa wito kwa vyombo vinavyohusika kuharakisha uchunguzi na hiyo itasaidia kukabiliana na kupunguza matukio ya namna hii,” amesema.

Mkuu wa Mkoa wa Dr es Salaam, Paul Makonda amesema haiwezekani kuzuia kifo lakini kwa mazingira yalichosababisha kifo cha Aquilina ndiyo yanaacha maswali na leo tumekusanyika.

“Namshukuru Paroko kwa kutukumbusha kuwa wapatanishi na kutuhimiza kulinda amani kila mwananchi ana wajibu wa kuilinda amani.

“Imani yangu Jeshi la Polisi litatupa majibu litakapokamilisha upelelezi lakini nawasihi wengine kujiepusha na kurusha maneno badala ya kukaa pamoja kama nchi, nasisitiza tuwaache wenye mamlaka wafanye uchunguzi na sisi tuishi kama taifa na ndugu,” amesema Makonda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles