30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

ASKOFU KKKT ASEMA KUTENGANISHA DINI, SIASA HAIWEZEKANI


NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli (K.K.K.T) Dayosisi ya Karagwe, Askofu Benson Bagonza, amesema amani ni jambo linalopaswa kuhubiriwa na vyama vya siasa na taasisi za dini.

Amesema kwamba huwezi kusema viongozi wa dini wasishiriki katika siasa wakati kila kitu wanachofanya kinatokana na siasa.

Askofu Bagonza alisema hayo Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), ambao ulihuisha pia viongozi wa dini.

Alisema viongozi wa dini wana wajibu wa kushauri na kuonya pale wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani, hivyo kujitenganisha na siasa haitawezekana.

“Hatuwezi kukaa katika nchi kama tupo peponi, yapo matukio ya uvunjifu wa amani ambayo yanatokea yanayohusu uvunjifu wa amani nchini lazima tukemee.

“Kauli hii ni ibada ya sanamu, hili shati nililovaa bei inapangwa na wanasiasa, kukubali kununua  nimeshashiriki siasa, ni kitu kisichowezekana unakula, unalala, unaamka hii ni siasa, kwa hiyo tunaishi katika nchi ya siasa.

“Kanisa lina nguvu karibu miaka 2,000, hivi vyama hakuna kilichofika hata miaka mia, maana hii habari ya viongozi wa dini kuongelea siasa imekuwepo  kwa miaka  2,000 sasa,” alisema Askofu Bagonza.

Alisema maendeleo bila siasa ni kujidanganya.

“Ilani zinatungwa na wanasiasa, huwezi kutenganisha siasa na …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles