AFAULU SEKONDARI KWA KUSAIDIWA KUSOMA, KUANDIKA

0
1351

Mwanafunzi Jackson James wa kidato cha kwanza, Shule ya Sekondari Mtwara Ufundi, ambaye ni mlemavu wa viungo, hajui kusoma wala kuandika lakini amefaulu kuingia sekondari.

Aidha, mwanafunzi huyo anahitaji msaada wa kwenda Hospitali ya Mifupa na Macho (CCBRT), kwa ajili ya mazoezi ya viungo vyake vya mwili ili aweze kuendelea na masomo yake.

Akimzungumzia mwanafunzi huyo Mkuu wa shule hiyo, Paul Kaji amesema mwanafunzi huyo hajiwezi kwa kila kitu hata kuandika hawezi lakini kicha ya ulemavu wake amefaulu katika shule hiyo na amekuwa akisomewa na kusaidiwa na wenziwe.

“Amekuwa akisaidiwa kusoma na kuandika tangu huko alikotoka na hadi sasa utaratibu huo unaendelea tatizo linakuja pale anaposhindwa kujigemea mwenyewe kwa kila kitu, tunawaomba wasamaria wema kumsaidia ili aweze kuendelea na masomo kwani uwezo anao,” amesema Kaji.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here