29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

JINSI SARATANI YA BEGA ILIVYOMALIZA UHAI WA MARIAM

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

UGONJWA wa saratani ya bega uliosambaa katika viungo vingine vya mwili ikiwamo mbavu, mifupa na mapafu ndio uliosababisha kifo cha mtoto Mariam Amrima (17).

Mariam ambaye ni mkazi wa Masasi mkoani Mtwara, alikuwa anakabiliana na maumivu makali kutokana na uvimbe mkubwa ulioota katika eneo la bega lake la kulia.

Alifariki dunia alfajiri ya jana akipatiwa matibabu dhidi ya ugonjwa huo katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI).

Taarifa za kifo cha Mariam zilithibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk. Julius Mwaiselage, alipozungumza na MTANZANIA Jumapili kwa simu.

“Ni kweli amefariki leo (jana) alfajiri, hali yake ilibadilika ghafla usiku, alikuwa anashindwa kupumua vizuri, madaktari na wauguzi wetu walijitahidi kumsaidia, hata hivyo ilipofika alfajiri alifariki dunia,” alisema.

Dk. Mwaiselage alisema mtoto huyo alicheleweshwa kufikishwa hospitalini kwa matibabu hali iliyosababisha ugonjwa wake kusambaa zaidi.

“Uchunguzi ulibaini ugonjwa ulikuwa umefika hatua ya nne ambayo ni hatua ya …………………

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles