29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI WAZUIA MKUTANO WA ZITTO JIMBONI

Na MWANDISHI WETU-Kigoma


JESHI LA Polisi mkoani Kigoma limezuia mkutano wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), aliokuwa aufanye Uwanja wa Mwanga Centre mjini hapa.

Mkutano huo uliokuwa ufanyike jana ulizuiwa na Polisi kupitia barua yenye kumb KIG/A.24/60/ACT/VOL.1/105 kwenda kwa mbunge huyo na kusainiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kigoma (OCD), M.R. Mayunga.

Kutokana na zuio hilo, Zitto alisema wamefanya kazi kubwa jimboni kipindi cha karibuni, kuanzia utatuzi wa suala la kodi kwa wafanyabiashara, masuala ya hifadhi ya jamii kwa vikundi, uhamasishaji wa uanzishwaji wa viwanda vidogo vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

“Pamoja na uzinduzi wa kampeni ya upandaji michikichi 1,500,000 katika mkoa mzima wa Kigoma. Nilipanga kuzungumza na wananchi wenzangu kuwaeleza haya yote, pamoja na kuhamasisha upandaji michikichi katika manispaa yetu.

“Jeshi la polisi limezuia mkutano wangu wa hadhara kama Mbunge wa Kigoma Mjini kinyume na sheria ya Bunge ya mwaka 1988. Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inalazimisha (kwa kutumia neno shall ) mbunge kufanya mkutano kwenye jimbo lake bila vikwazo.

“…mimi sitaki kuwapa polisi sifa ya kupambana nasi. Tumeahirisha mkutano mpaka siku ya jumamosi lakini tumewaandikia barua rasmi kuwa sheria waliyoinukuu sio sheria halali na haihusiani na mikutano ya mbunge kwenye jimbo lake la uchaguzi. Sheria wanayopaswa kunukuu ni sheria namba 3 ya mwaka 1988 kifungu cha 4(1),” alisema Zitto,

Alisema ofisi yake itamwandikia barua Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu suala hilo ili lisifanyike kwa mbunge mwengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles