32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ukawa: Takukuru ikunjue kucha zake

???????????????????????????????NA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imetakiwa kukunjua kucha zake kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema sasa umefika wakati kwa Takukuru kuhakikisha wanadhibiti matumizi ya fedha kwa wagombea wanaotangaza nia katika vyama mbalimbali.
Profesa Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), alisema ni lazima Mkurugenzi wa Takukuru, Dk. Edward Hosea, aeleze mikakati yake ya namna atakavyopambana na rushwa, hasa kwa wagombea ambao si waadilifu na ambao wamekuwa wakitumia fedha.
“Ni muhimu katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu, Dk. Hosea akaelezea mikakati yake ya kupambana na wanaowania uongozi ambao wanakiuka maadili ili waeleze fedha wanazotumia wanazitoa wapi. Na jambo hili liwe kwa vyama vyote,” alisema Profesa Lipumba.
Akizungumzia uteuzi wa wagombea ubunge na urais kupitia Ukawa, alisema hivi sasa kila chama kipo katika mchakato wa ndani kwa ajili ya kukamilisha taratibu zake.
“Ukawa (mchakato) unaendelea vizuri, nami nimetangaza nia ndani ya chama changu kwa nafasi ya urais, nasubiri mkutano mkuu wa chama chetu ndiyo utatoa uamuzi wa mwisho.
“Tukishakamilisha kazi hii kwa kila chama sasa ndiyo kamati maalumu ya viongozi itaketi kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na Ukawa na kisha utatoa na jina la mgombea mmoja wa urais ambaye atapambana na vyama vingine,” alisema Lipumba.
Alizungumzia pia utendaji kazi na weledi wa taasisi za Serikali ikiwamo Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), ambao walichunguza tukio la kupigwa kwa viongozi na wafuasi wa CUF Januari 27, mwaka huu wakati walipokuwa wanakwenda kuahirisha mkutano wa hadhara.
Ripoti iliyotolewa na tume hiyo, ilieleza kwa kina namna Jeshi la Polisi lilivyotumia nguvu kupita kiasi na hata kusababisha majeruhi kadhaa kinyume cha sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles