25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

WANANCHI WAOMBWA KUCHANGIA DAMU KWA HIYARI

Na RENATHA KIPAKA-BUKOBA


MKUU wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu, ameyataka mashirika mbalimbali pamoja na wananchi kujitolea katika zoezi la kuchangia damu kwa hiyari.

Alitoa kauli hiyo juzi wakati akipokea vinywaji kutoka katika tasisi za kifedha za CRDB, NMB pamoja na kiwanda cha kahawa Tanica ambapo alisema  kuchangia damu kuna faida kubwa sana  ikiwemo kufahamu hali ya afya pamoja na kujua kundi la damu ulilonalo.

“Niwatake wananchi wote pamoja na mashirika kushiriki katika kampeni hii kwa hiyari ili kila mtu ahusike katika kuhakikisha hosipitali zetu zina akiba ya kutosha ya damu,” alisema Kijuu.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera, John Mwombeki, alisema malengo ya kuwepo kampeni hiyo ni maandalizi ya kuwa na damu ya kutosha katika kipindi hiki cha sikukuu kwani kipindi hicho kuna  wahitaji wengi wa damu hivyo maandalizi ya kutosha yanahitajika.

“Damu inayohitajika ni uniti 900, hivyo kila wilaya inatakiwa kukusanya uniti 100 na kwa timu ya mkoa nayo inatakiwa kuwa na uniti 100 ambayo itasaidia kupunguza uhitaji wa damu,” alisema Mwombeki.

Mwombeki alisema damu imekuwa ikipatikana shuleni na katika majeshi sasa mwanafunzi wapo likizo na majeshi pia wapo likizo, hivyo itakuwa vigumu kuwasaidia wahitaji usipofanyika utaratibu mapema na kuwaomba wananchi mmoja mmoja kujitokeza ili kuchangia damu kwa hiyari.

“Kama tunavyojua wahitaji wakuu wa damu ni akina mama wanaofanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua, watoto wenye umri chini ya miaka mitano pamoja na wahanga wa ajali za pikipiki na magari, hivyo damu ni muhimu sana,” alisema Mwombeki

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles