NA CHRISTOPHER MSEKENA
TUKIWA tumebakiza Jumatatu moja tu kuumaliza mwaka 2017, Juma3tata tunakusogezea matukio ya Vvizazi na vifo vilivyotokea kwenye tasnia ya burudani hapa Bongo.
Kwa kuanza tuanze na matukio ya vizazi ambapo nakukutanisha na mastaa mbalimbali waliobahatika kupata watoto mwaka huu wa 2017, tunaanza na,
MILLEN MAGESE
Licha ya kufanyiwa upasuaji zaidi ya mara 13 kwenye kizazi chake kufuatia kusumbuliwa na ugojwa wa Endometriosis, mrembo huyu Julai 13 mwaka huu alijifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume anayeitwa Kairo.
Mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2001, kwake ilikuwa ni kama muujiza kwani ni asilimia ndogo ya waathirika wa ugonjwa huo huwa wanashika ujauzito na kujifungua salama.
LINAH
Julai 25 mwaka huu, staa wa Bongo Fleva, Esterina Sanga ‘Linah’ naye alipata mtoto wa kike anayeitwa Tracey Paris, huku mzazi mwezie akiwa ni meneja wake ambaye ni mwongozaji wa video anayefahamika kwa jina la Ghost.
FAIZA ALLY
Agosti 3 mwaka huu mwanamitindo ambaye ni mzazi mweza wa mkongwe wa muziki wa Hip Hop na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally alipata mtoto wa pili wa kiume anayeitwa Li, aliyezaa na mpenzi wake anayedai ni Mmarekani mweusi.
HAMISA MOBETTO
Agosti 8 mwaka huu, mwanamitindo na msanii wa filamu, Hamisa Mobetto aligosnga vichwa vya habari za burudani baada ya kujifungua mtoto wa pili anayeitwa Dylan, mtoto aliyezaa na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na kuzua gumzo kwani staa huyo wa muziki alikiri kuchepuka kwenye uhusiano wake imarara na Zari The Boss Lady.
Hamisa Mobetto ni mama wa watoto wawili, mtoto wake wa kwanza wa kike anaitwa Fantansy na wa pili ndiyo huyo, Dylan.
ESHA BUHETI
Ambaye ni msanii wa filamu, Agosti 8 mwaka huu alifanikiwa kupata mtoto wa pili wa kike anayeitwa Claribell.
NAVY KENZO
Hili ni kundi la muziki linaloundwa na wasanii wawili, Nahreel na Aika ambapo, Desemba 9 mwaka huu walifanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume anayeitwa, Gold.