32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

UJERUMANI YAGUNDUA AKAUNTI BANDIA ZA WACHINA

BERLIN, UJERUMANI


SHIRIKA la Ujasusi la Ujerumani (BfV), limechapisha taarifa za watumiaji wa mitandao ya jamii linalosema ni majina bandia yanayotumiwa na majasusi wa Kichina kukusanya taarifa kuhusu maofisa na wanasiasa wa Ujerumani.

BfV ilichukua hatua hiyo isiyo ya kawaida kwa kuwataja majina watumiaji wa mitandao ya jamii na taasisi bandia ili kuwaonya maofisa wa Serikali juu ya kitisho cha kupenyeza taarifa muhimu kupitia mitandao hiyo.

“Majasusi wa Kichina wako kwenye mitandao kama vile Linkedln na wamekuwa wakijaribu kwa kitambo kirefu kukusanya taarifa na kupata vyanzo vya kijasusi kwa njia hii, ikiwamo kusaka taarifa za tabia za watumiaji, mambo wanayopendelea na mwamko wao kisiasa,” limesema shirika hilo la ujasusi wa ndani.

BfV imesema katika miezi tisa ya utafiti wake, imegundua zaidi ya raia 10,000 wa Kijerumani wamewahi kutafutwa kupitia mtandao wa Linkedln na akaunti bandia ambazo zinajitambulisha kama washauri, wataalamu, wabunifu ama wasomi.

Kwa mujibu wa maofisa wa BfV, inawezekana kuna idadi kubwa zaidi ya watu waliolengwa na akaunti bandia ambazo bado hazijatambuliwa.

Akizungumza mjini Beijing juzi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Lu Kang, alisema shutuma hizo hazina msingi wowote.

“Tunatarajia taasisi sahihi za Kijerumani, hasa idara za Serikali, zinaweza kusema na kutenda mambo kwa utaratibu na si kufanya vitu ambavyo havina faida kwa maendeleo ya mahusiano kati ya pande hivi mbili,” alisema Lu.

Miongoni mwa akaunti bandia ambazo taarifa zake zilichapishwa na BfV, ni ya ‘Rachel Li’ anayejitambulisha kama kiongozi wa taasisi ya RiseHR na ‘Alex Li’ anayejitambulisha kama meneja miradi kwenye Kituo cha Utafiti kati ya Ulaya na China.

Nyingi kati ya akaunti hizo zina picha za vijana warembo wa kike na wa kiume.

“Picha ya ‘Laeticia Chen’, meneja kwenye Kituo cha Siasa za Kimataifa na Uchumi ilitolewa kutoka mtandao wa warembo,” aliasema ofisa mmoja wa BfV.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles