25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

MCHUNGAJI ALIYESHTAKIWA KWA UHAINI AACHIWA

HARARE, ZIMBABWE


MAHAKAMA ya Zimbabwe imemuachia huru, Mchungaji Evan Mawarire aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya uhaini.

Mchungaji Mawarire alifunguliwa mashtaka ya uhaini na Serikali ya ya Rais Mstaafu, Robert Mugabe.

Akisoma hukumu iliyomuachia huru mchungaji huyo jana, Jaji wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe, alisema upande wa serikali haukutoa ushahidi dhidi ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili.

Baada ya kuachiwa, mchungaji Mawarire aliwaambia waandishi wa habari kuwa amefurahishwa na uamuzi wa mahakama na kwamba wakati kesi yake ikisilizwa ulikuwa wa ajabu na pia hakupaswa kukamatwa.

Aidha, alimtaka Rais Emmerson Mnangagwa kuheshimu haki za binadamu vinginevyo raia wataandamana iwapo watabaini serikali mpya inakiuka uhuru wao.

“Huu unaweza kuwa ushahidi wa Zimbabwe huru, lakini kesi hii haikuwa na kichwa wala miguu. “Lakini pia nadhani ni mapema kuthibitisha iwapo mahakama iko huru bila kuingiliwa wa serikali,” alisema Mchungaji Mawarire.

Alisema kwa miaka mingi mahakama nchini humo zilionekana kama chombo cha kukandamiza uhuru wa kisiasa kwa wapinzani wa Serikali ya Zimbabwe.

Mchungaji Mawarire alikuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Mstaafu Mugabe, aliyelashinikizwa na chama chake na jeshi kuachia ngazi baada ya kukaa madarakani kwa miaka 37.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles