29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

KAFULILA AIKACHA CHADEMA, ADAI HANA IMANI NA UPINZANI

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (2010-2015), David Kafulila amejivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokana na kutokuwa na imani na upinzani katika kupambana na ufisadi.

Kafulila anakuwa mwanachama wa tatu wa Chadema, kujiondoa katika chama hicho ndani ya wiki moja ambapo wiki iliyopita aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Laurence Masha na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama hicho, Patrobas Katambi kujiondoa na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana.

Hata hivyo, Kafulila amesema bado anatafakari na hivi karibuni atatangaza jukwaa jipya akimaanisha chama atakachohamia ili kuendeleza harakati zake dhidi ya ufisadi.

Sababu nyingine aliyoitaja kumuondoa Chadema ni upinzani kukosa ajenda ya ufisadi kutokana na Rais John Magufuli kwa vitendo hasa baada ya watuhumiwa na wahusika wa rishwa kubw akufikishwa mahakamani ambapo matokeo ya tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na mashirika huru ya ndani na nje ya nchi kyanaonyesha kiwango cha rushwa nchini kimeporomoka.

“Nikiwa mmoja wa wanasiasa vijana nilibahatika kutumikia Bunge la 10, siku zote nimejipambanua na kujitoa mhanga kupambana na ufisadi kupitia jukwaa la bunge, vyama vya siasa na shughuli mbalimbali za kijamii kwa ujumla.

“Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni na hasa tangu harakati za uchaguzi mwaka 2015 vyama vya upinzani nchini vibnaonekana kuoigwa ganzi na kupooza katika juhudi zake za kuopambana na ufisadi, ghafla ufisadi siyo tena ajenda kuu ya upinznai nchini kwa sababu ni wazi kuwa upinzani siyo tena jukwaa la kuendesha vita dhidi ya ufisadi,” amesema Kafulila katika taarifa yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles