29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

DAKTARI AKAMATWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Na SAFINA SARWATT-KILIMANJARO

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imemkamata daktari wa Hospitali ya Rufaa, Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro, Holle Makungu, alisema jana katika taarifa yake  kwamba daktari huyo, Deogratias Urio, alikamatwa Novemba 15, mwaka huu  baada ya taasisi hiyo kupokea malalamiko kutoka kwa ndugu wa mgonjwa.

Kwa mujibu wa Makungu, Urio anadaiwa kupokea rushwa ya 150,000 kutoka kwa ndugu wa mgonjwa aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji hospitalini hapo.

“Tulipokea malalamiko kutoka kwa ndugu wa mgonjwa aliyekuwa akipigwa danadana kupatiwa huduma ya upasuaji hospitalini hapo.

“Katika tukio hilo, daktari huyo alikamatiwa  katika Mji Mdogo wa Himo akiwa kwenye baa maarufu ya Mombasa High Way baada ya kuwekewa mtego na makachero wetu.

“Mgonjwa alikuwa akihitaji kufanyiwa upasuaji wa uvimbe katika kizazi chake tangu Oktoba mwaka huu  baada ya kufanyiwa vipimo katika hospitali hiyo na kugundulika ana uvimbe.

“Pamoja na kubainika ana uvimbe huo, mgonjwa hakuweza kupata tiba haraka baada ya kuelezwa na daktari huyo  kwamba hawezi kutibiwa hadi atakapotoa fedha hizo.

“Kwa hiyo  tunaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo kabla ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

“Pamoja na hayo, tunawaomba madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Mawezi na kwingineko mkoani hapa  wazingatie viapo vyao ili hospitali zetu ziwe mfano wa kuigwa katika utoaji wa huduma,” alisema Makungu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles