HOMA ya ini (hepatitis) ni neno linalotumika kujumuisha magonjwa yanayoleta madhara kwenye ini.
Madhara haya hushambulia na kudhuru seli za ini. Ugonjwa huu unaweza kupona wenyewe bila kuleta madhara makubwa au unaweza kuwa mkubwa kiasi cha kuacha makovu kwenye maini.
Mara nyingi ugonjwa huu ukiwa mkubwa uwa unamsumbua mgonjwa kwa kipindi kinachoweza kufikia hadi miezi sita. Ni ugonjwa unaoweza pia kuwa wa muda mrefu zaidi.
Kuna aina kuu tano za ugonjwa huu na aina hii zote huletwa na virusi,karibu watu milioni 250 duniani wameshambuliwa na hepatitis C wakati watu wapatao milioni 300 ni wale wanaoweza kueneza ugonjwa hepatitis B bila wao wenyewe kudhurika (hepatitis B carriers).
Aina nyingine za ugonjwa huu ni hepatitis A,D na E. Uharibifu mkubwa wa maini ya binadamu hutokana na aina tatu za virusi wa hepatitis, hepatitis A,B na C.
Hepatitis ambayo haitokani na virusi huitwa hepatis X. Kuna aina ya ugonjwa wa homa ya ini unaotokana na kirusi wa aina ya kipekee kabisa (HGV) nayo huitwa hepatitis G.
Kuna aina nyingi za hepatitis ambazo haziambukizi.
Sababu za kupata ugonjwa wa ini ni pamoja na unywaji wa pombe, utumiaji wa madawa na kemikali.
Mtu pia anaweza kupata maradhi haya kwa kurithi kwenye ukoo wenye historia ya maradhi hayo.
Kutokana na hitilafu katika utendaji kazi wa mwili au kutokana na kuharibika kwa kinga zake za mwili.
Ulafi waweza kuwa chanzo cha madhara kwenye ini. Homa za ini kutokana na vitu hivi haziambukizi kutoka mtu mmoja hadi kwa mwingine.
Kazi za ini
Ini ni kiungo kikubwa kuliko kingine cho chote kile kilicho ndani ya mwili wa binadamu.
Ini huwa na uzito upatao kilo 1.36,ini limegawanyika katika vipande vinne vyenye ukubwa na urefu tofauti.
Damu hulifikia ini kupitia hepatic artery na potal vein. Hepatic artery huchukua damu yenye oksijeni kwa wingi kutoka aorta na kuifikisha ndani ya ini.