25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

MALEZI YA KUTANGATANGA YANAHARIBU MTOTO

Na Aziza Masoud

MFUMO wa malezi wa wazazi wa sasa kwa watoto unaonekana kubadilika, tofauti na ilivyokuwa zamani.

Kipindi cha nyuma wazazi walikuwa makini zaidi katika malezi, ikiwa ni pamoja kuhakikisha anakuwa karibu na mtoto, anajua anafanya nini na katika mazingira gani, ili kuepuka kuchangamana na watoto wasiokuwa na maadili mazuri.

Hali hii imekuwa tofauti kidogo kwa wazazi wa siku hizi, baadhi wamekuwa tofauti kulingana na utaratibu wa malezi waliyojiwekea kwa  watoto wao.

Kutokana na hali ya maisha na mazingira anayokuwa nayo mzazi katika eneo husika, ikiwamo kukosa muda wa kumwangalia mtoto kwa sababu ya kutingwa na shughuli mbalimbali za kutafuta kipato,  wapo ambao wanawatumia wadada wa kazi kwa ajili ya kuangalia watoto, lakini wapo pia wanaoishi kwa kuwahamisha watoto kwenda kuishi kwa ndugu na jamaa ambao wanakuwa karibu.

Wazazi wanawahamisha watoto kwenda kwa ndugu mbalimbali ili kupata msaada wa malezi, tunaweza kusema wanawalea watoto malezi ya kutangatanga, wana hatari ya kuharibu watoto wao kitabia.

Japokuwa wapo ambao wanakuwa na sababu ya kufanya hivyo kwa muda mchache, mfano anakaa katika nyumba ambayo haina nafasi, hana dada wa kazi, hivyo hakuna mtu  wa kumwangalia motto, hali hiyo ikikukuta unaweza ukampeleka kwa ndugu kwa ajili ya kupata uangalizi kipindi unapokuwa katika mihangaiko.

Lakini wapo wazazi ambao wamejiwekea utaratibu wa kuwa mtoto wake ana uwezo wa kuishi kila nyumba, utakuta mtoto wake hatulii nyumba moja, leo kalala  kwa mjomba, kesho kwa shangazi na siku nyingine kwa dada.

Malezi ya namna hii ni hatari kwa sababu yanaweza kuchangia kumharibu mtoto, kwanza yanamchanganya, sababu katika kila nyumba anakokwenda kukaa kuna taratibu zake na watoto wa eneo husika wanakuwa na tabia tofauti.

Ipo nyumba ambayo itamfanya mtoto wako awe na maadili mazuri, lakini zipo baadhi ambazo zina watoto wana tabia mbaya mpaka wameshindikana na wazazi, hizo ndizo za kuziogopa.

Mzazi unapaswa kutambua kuwa, mtoto akiwa anashinda kwenye nyumba ya watoto ambao ni wezi na yeye lazima watamfundishia kuiba, hata kwakumpa vitu vidogo vidogo.

Tabia hizi anaweza kuja kuwa nazo mpaka ukubwani na kumfanya kuonekana kijana mtukutu, huku jamii yote ikikutolea macho mzazi kwamba umeshindwa kumlea.

Wazazi ni vema kila mtu akalea mtoto wake, endapo litatokea tatizo ambalo litasababisha ushindwe kukaa na mtoto wako kwa wakati huo, ni vema utafute nyumba salama ambayo haitamharibu mtoto wako kwa njia yoyote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles